BREAKING:MOTO WATEKETEZA MADUKA ZAIDI YA 10 DAR
Jan 5, 2026
MOTO mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza maduka 11 ya bidhaa mbalimbali yakiwemo ya nguo na matairi, eneo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Januari 05, 2025.
Mashuhuda wameueleza mtandao wa Matukio Daima kuwa hadi sasa hawajui chanzo cha moto huo.
Sofia Mligo Mrakiribu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kinondoni na Ubungo, amelielezea tukio hilo jinsi lilivyotokea.
