Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
FORLAND WASAINI HATI YA MAKUBALIANO [MoU] NA SERIKALI YA TANZANIA UHIFADHI MISITU

FORLAND WASAINI HATI YA MAKUBALIANO [MoU] NA SERIKALI YA TANZANIA UHIFADHI MISITU

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima  NJOMBE 

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Finland imesaini hati ya makubaliano ya kikanda [MoU] chini ya mradi wa maendeleo ya matumizi ya ardhi na minyororo ya thamani ya misitu Tanzania [FORLAND] ili kuimarisha usimamizi na uratibu wa mandhari ya misitu katika maeneo ya mradi.


Mkataba huo umesainiwa mkoani Njombe ukihusisha mikoa ya Iringa na Njombe ambapo jumla ya vijiji 46 vya mkoa wa Njombe na vijiji 26 vya mkoa wa Iringa vitahusika katika utekelezaji wa mradi huo unaokwenda kutekelezwa katika nyanja tofauti zikiwemo za uzalishaji wa mbegu bora za miti,mikakati ya mapambano ya moto na utoaji elimu kwa wakulima wa miti.



Mratibu wa mradi wa FORLAND toka wizara ya Maliasili na utalii Bi.Emma Nzunda anatumia fursa hiyo kusisitiza mashirikiano ya karibu kati ya pande zote za utekelezwaji wa mradi huo.


Mshauri mkuu wa kiufundi wa mradi wa FORLAND toka Nchini Finland bwana Michael Howkes anasema mradi huo utahusisha mnyororo mzima wa zao la misitu kuanzia wakulima wenyewe,wasafirishaji viwanda vya uchakataji pamoja na kuwajengea uwezo wadau wa misitu.


Serikali za mikoa ya Njombe chini ya kaimu katibu tawala mkoa Mhandisi Joseph Mutashubila ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika zoezi hilo na Nuru Sovela Kaimu katibu tawala mkoa wa Iringa zinakiri kuwapo kwa majanga ya moto yanayowarudisha nyuma wakulima na uchumi hivyo mkataba huo uende kuwa mwarobaini wa kilimo cha miti.


Naye mratibu wa Kongani ya Iringa wa mradi wa FORLAND Nyachia Robert anasema mikakati ya kukabiliana na majanga ya moto kwenye misitu ni miongoni mwa mambo yanayokwenda kutekelezwa ndani ya mradi huo.


Kwa upande wao wadau wa misitu nchini wanasema mradi huo uwanasue wakulima wa mitu kwenye madhira mbalimbali wanayokumbana naye hususani kwenye upande wa mbegu feki na majanga ya moto.


Kusainiwa kwa Mkataba huu kuna akisi dhamira ya pamoja ya wadau wote katika kukuza mandhari endelevu ya misitu,kuboresha maisha ya wananchi na kuchangia katika malengo ya kitaifa na kimataifa ya tabianchi na uhifadhi wa banuwai.




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3