MADURO NA MKEWE WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO
Jan 5, 2026
Dunia inashuhudia historia mpya muda huu na ni ajabu, Leo rasmi Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, ameonekana akisafirishwa chini ya ulinzi mzito wa Polisi wa Marekani na Kikosi Maalum cha Kuzuia Dawa za Kulevya (DEA) kutoka mahabusu ya Brooklyn kuelekea Mahakama ya Shirikisho Manhattan, New York.
Msafara huo uliotawaliwa na magari meusi, helikopta na askari wenye silaha nzito, umemfikisha Maduro mahakamani hapo kusomewa mashitaka mazito
Maduro alikamatwa Januari 3, 2026, katika operesheni ya kijeshi iliyoongozwa na Marekani jijini Caracas, ikiwa ni utekelezaji wa sera mpya na kali ya Rais Donald Trump akimshughulikia aliyemuita Dikteta.
Je, hii ni Haki inatendeka au ni Ubabe wa Marekani? Tupe maoni yako.


