TANZIA:MKE WA JAH PEOPLE AFARIKI DUNIA
Jan 20, 2026
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga maarufu kwa jina la "Jah People", amepatwa na msiba wa kufiwa na mke wake Rozana Kapasi.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Marehemu Rozana amefariki dunia alfajiri ya leo, Januari 20, 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph (Ikelu). Taarifa hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe, Justin Nusulupila, pamoja na watu wa karibu wa familia.
Familia imeomba utulivu na dua katika kipindi hiki cha majonzi, huku ikiahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi na taratibu nyingine za msiba kadri zitakavyokuwa tayari.
