TUNAJIANDAA KUISHAMBULIA TENA VENEZUELA ISIPOJIHESHIMU -TRUMP
Jan 4, 2026
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa, wanajiandaa kufanya shambulio la pili nchini Venezuela, endapo viongozi wa nchi hiyo hawatokuwa na heshima.
Awali Mahakama ya nchi hiyo ilimtangaza aliyekuwa Makamu wa Rais Delcy Rodríguez kuwa Rais wa mpito wa Venezuela, ambapo katika hotuba yake Rodríguez alisema kwamba Maduro bado ni Rais huku akiitaka Marekani kumuachia huru.
Afisa mkuu wa Venezuela alisema serikali inabaki kuwa na umoja na kumuunga mkono Nicolás Maduro licha ya kukamatwa kwake.
