WANAFUNZI WA CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA WAKIWA ZIARA YA MAFUNZO IRINGA
Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mkoani Mbeya wamefika katika Mkoa wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kimasomo.
Akizungumza na Matukio Daima Media Mkufunzi wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya Marco Nassary alisema wapo mkoani Iringa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika kozi ya usanifu majengo kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo.
Nassary alisema kuwa katika mitaala yao wanafunzi baada ya kusoma darasani nadharia kwa muda wa wiki saba wanapata fursa ya kuweza kupita mtaani kwenda kuangalia mazingira halisi ya vitu walivyovisoma na kuvifanya kwa vitendo.
“Tupo katika mitaa mbalimbali ya mkoa wa iringa kwa ajili ya kuangalia maeneo mbalimbali ya kistoria na kuweza kujifunza historia mbalimbali katika usanifu majengo ili kuweza kujifunza kwa vitendo”alisema
“Wanafunzi tunawapeleka katika mikoa tofauti kulingana na ngazi wanayosoma hawa tulionao hapa tumewaleta iringakwa sababu iringa inautajili mwingi wa majengo ya kistoria mbalimbali hasa katika historia ya majengo mbalimbali na tunajifunza kupitia mijengo miji”alisema





















































