WATU WATATU WAKAMATWA MORO KWA TUHUMA ..
Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp
JESHI la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa Matukio tofauti ya mauaji na ukatili wa kijinsia yaliyotokea maeneo mbalimbali mkoani Morogoro .
Moja kati ya Matukio hayo ni kukamatwa kwa Helakimu Kacheli(50) aliyemuua mkewe Sofina Alipisin(27) kwa kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari, kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama alisema tukio la kwanza mtuhumiwa Kacheli alikamatwa Januari 4,2026 akijaribu kujiua kwa kujikata Koromeo kwa silaha Kali.
Kamanda Mkama alisema mtuhumiwa Kacheli ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha Sesenga ambapo marehemu mkewe ni mkulima na mkazi wa Lumbachini na mtuhumiwa baada ya kutekeleza tukio hilo na kujaribu kujiua aliokolewa na Sasa anaendea na matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Katika tukio linguine la Januari 5,2026,kamanda Mkama alisema alikamatwa Justine Thomas(42) mkazi wa Kitongoji cha Sogeambele kijiji cha Bonye kata ya Bwakila chini, tarafa ya Bwakila wilaya ya Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Machafu Magembe Masanja(42) baada ya ugomvi uliohusiana na mauzo ya mpunga bila ridhaa yake.
Aidha katika tukio lingine , Andrew Joseph Katanga(33) mkazi wa Katinduuka Wilaya ya Kilombero alikamatwa kwa tuhuma ya kumbaka mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.
Alisema tukio lilitokea Desemba 31,2925 ambapo baba huyo ilidaiwa alimfungia mtoto huyo chumbani kwake na kumuingilia kinguvu.
Kamanda Mkama alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia Sheria mkononi na badala yake watoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama ili Matukio ya kiuhalifu yazuiwe mapema kabla hayajaleta madhara.
