Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BREAKING:RAIS WA VENEZUELA NA MKEWE WAKAMATWA NA MAJESHI YA MAREKANI

BREAKING:RAIS WA VENEZUELA NA MKEWE WAKAMATWA NA MAJESHI YA MAREKANI

 



Marekani imeishambulia Venezuela na kumkamata Rais wake, Nicolas Maduro, ambaye ameondolewa nje ya nchi hiyo, Rais Donald Trump amesema leo Jumamosi Januari 3, 2026.

Kwa mujibu wa Reuters, Marekani haijafanya uingiliaji wa moja kwa moja wa aina hiyo katika Amerika ya Kusini tangu uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliomwondoa madarakani kiongozi wa kijeshi, Manuel Noriega.

"Marekani imefanikiwa kutekeleza shambulio kubwa dhidi ya Venezuela na kiongozi wake, Rais Nicolas Maduro, ambaye yeye pamoja na mke wake wamekamatwa na kusafirishwa kwa ndege kuondolewa nje ya nchi," Trump amesema katika chapisho lake kwenye mtandao wa Truth Social.

Hakukuwa na uthibitisho kutoka kwa Serikali ya Venezuela.


Marekani imekuwa ikimtuhumu Maduro kwa kuendesha "nchi ya mihadarati" na kuiba kura katika uchaguzi.

Kiongozi huyo wa Venezuela, aliyerithi madaraka kutoka kwa Hugo Chavez mwaka 2013, alisema Washington inataka kudhibiti akiba ya mafuta ya nchi hiyo, ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3