Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BARAKA AKAMATWA LODGE NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

BARAKA AKAMATWA LODGE NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia kijana mmoja, Baraka Juma (19), mkazi wa Kagongwa, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumtorosha binti mwenye umri wa miaka 14, mwanafunzi wa kidato cha pili, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na polisi, mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio hilo Januari 05, 2026 katika Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, ambapo alimdanganya na kumtorosha mwanafunzi huyo kinyume cha sheria.

Katika taarifa hiyo inaelezwa kuwa baada ya kufanyika ufuatiliaji wa kina, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Januari 17, 2026, katika nyumba ya kulala wageni eneo la Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na mwanafunzi huyo, wakati wakijiandaa kusafiri kuelekea Kagongwa, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Polisi imeeleza kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa sheria za nchi.

SACP Faustine Mafwele amesisitiza kuwa polisi haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya uhalifu, hususan vinavyohusisha ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3