POLISI WATOA UFAFANUZI VIDEO YA ASKARI KUTAKA KUPOKONYWA SILAHA NDANI YA BENKI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya limetoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikionesha Askari Polisi akipambana na mtu mmoja huku akiwa na silaha ya moto.
Taarifa sahihi ni kuwa, mnamo Januari 15,2026 majira ya saa nane mchana katika Benki ya CRDB tawi la Sirari - Tarime, mtu aitwaye John Kohe Amosi Mkazi wa Kijini cha Sokoni - Sirari, alifika katika benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja hadi kwa mtoa huduma wa benki (bankteller) kama mteja huku akiwa amebeba begi dogo na kumwamuru kwa nguvu mtoa huduma ampe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.
Hali hiyo ilisababisha wasiwasi ndani ya benki na kulazimu Askari Polisi waliokuwa lindo nje ya benki hiyo wajulishwe na wakamfuata mtu huyo na kumtaka atoke nje na alitii amri hiyo.
Wakati anasindikizwa na Askari kutoka nje ghafla alimvamia askari kwa lengo la kumpora silaha kwa kupambana na askari, hata hivyo askari walifanikiwa kumdhibiti na kumtoa nje ya benki bila kutumia silaha pamoja na kitendo alichofanya.
Aidha, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa, mtu huyu hana akaunti kwenye benki ya CRDB.
Uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini nia ya mtu huyo ilikuwa ni nini na alikuwa anasukumwa na kitu gani hadi kufanya aliyoyafanya ili hatua zingine za kisheria zifuate.
TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
