Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KAMPUNI YA G'S CONTRACTS LTD IRINGA YAPATA CHETI CHA PONGEZI NA JESHI LA POLISI, MKURUGENZI GAMBA ATOA WITO HUU

KAMPUNI YA G'S CONTRACTS LTD IRINGA YAPATA CHETI CHA PONGEZI NA JESHI LA POLISI, MKURUGENZI GAMBA ATOA WITO HUU


Mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James katikati akimkabidhi cheti cha shukrani kwa kuchangia maendeleo ya jeshi la polisi mkurugenzi wa kampuni ya G'S CONTRACTS LTD Stephen Gamba  wakati wa hafla ya Polisi Day Iringa 2026 kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa SACAP Allan Bulumbi 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA 

 Mkurugenzi wa kampuni ya G’S Contractors Ltd, Stephen Gamba, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama katika kudumisha amani na utulivu mkoani Iringa. 

Gamba ambae kampeni yake ilipata cheti cha shukrani toka jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kutambua mchango wa ushirikiano na uchangiaji wa maendeleo ya mkoa wa Iringa hasa kwa jeshi la polisi,alitoa Rai hiyo juzi wakati wa hafla ya Polisi Family Day Iringa 2026.


Alisema kuwa kazi inayofanywa na jeshi la polisi katika ulinzi wa Raia na Mali zao ni kubwa hivyo inapaswa kuungwa mkono. 

Hata hivyo Gamba aliwapongeza askari na watumishi waliopewa heshima tuzo kwa juhudi zao za kutimiza majukumu yao kwa uadilifu, huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama. 

Alisema kuwa mchango wa wadau wa sekta binafsi ni muhimu katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha amani na utulivu unadumishwa.

“Tunapoonyesha mshikamano na vyombo vya usalama, tunachangia moja kwa moja katika kuhakikisha usalama wa jamii unadumishwa na shughuli za kijamii na kiuchumi zinaendelea kwa ufanisi,” alisema Gamba.

Aidha, Gamba aliwahimiza wananchi kuheshimu na kutii sheria za nchi kwa alisema  kuwa ushirikiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi ni msingi wa kuimarisha amani, kwani linapofanyika, wananchi wanakuwa na mazingira salama ya kuendesha shughuli zao za kila siku.


 Alibainisha kuwa sheria na ushirikiano vinapofuatwa, mkoa unakuwa na hali ya amani na maendeleo yanayoweza kufanikishwa kwa urahisi.

Pia Gamba aliwataka wananchi kutambua nafasi ya kila mmoja katika jamii, kushirikiana na vyombo vya usalama, na kushirikiana na wadau wengine wa sekta binafsi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo haziingii na usalama haukiukiwi. 

Alisema kuwa ushirikiano huu ni nyenzo muhimu kwa serikali na wadau binafsi katika kufanikisha maendeleo endelevu.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James aliyekuwa mgeni rasmi katika Hafla hiyo alisema kuwa serikali inathamini mchango wa sekta binafsi katika jitihada za kudumisha amani. 

Kuwa Mchango wa G’S Contractors Ltd na wadau wengine unaonyesha jinsi ushirikiano baina ya wananchi, vyombo vya usalama, na sekta binafsi unaweza kuchangia kuimarisha usalama na kuhakikisha shughuli za kijamii na kiuchumi zinaendelea bila vikwazo

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3