MAREKANI YAISHAMBULIA VENEZUELA
Jan 3, 2026
Rais Donald Trump ameamuru Jeshi la Marekani kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas akitekeleza kile alichodai vitisho kutoka kwa kiongozi wa nchi hiyo, Nicolas Maduro.
Maofisa wa Marekani wamethibitisha kwa CBS News kuwa Rais alikuwa ametoa idhini ya mashambulizi hayo.
Mapema leo Jumamosi 3 Januari 2026, Serikali ya Venezuela imeishutumu Marekani kwa kushambulia vituo vya kiraia na kijeshi katika majimbo kadhaa.
Takriban milipuko saba na ndege zilizokuwa zikiruka chini ilisikika saa 2:00 asubuhi kwa saa za huko katika mji mkuu, Caracas.
Mtandao wa CNN umeripoti kuwa milipuko hiyo ilianza saa 1:50 asubuhi wanajeshi wakilenga Fort Tiona, ambako ndipo makao makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Venezuela.
Venezuela tayari imetangaza hali ya dharura kufuatia matukio hayo.
