Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KWA AJILI YA SALA NA DUA.

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KWA AJILI YA SALA NA DUA.

 

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza  Kafiti William Kafiti, amekutana na viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu pamoja na wazee  kutoka  kata 19 za Wilaya hiyo lengo likiwa kupata dua na sala ili aweze  kuanza rasmi majukumu yake ya kibunge akiwa amejikabidhi  mikononi mwa Mungu.


Akizungumza wakati wa mkutano huo, Kafiti alisisitiza umuhimu wa kumtanguliza Mungu katika kila jambo, hasa katika kipindi hiki cha kuanza majukumu yake ya kibunge.

"Safari yangu ya kibunge ni ya kwanza, na najua kuwa hakuna kitu kingine kitaweza kufanikisha kile ninachokusudia bila kumtanguliza Mungu, Wakati wa kampeni tulianza na Mungu, tukamaliza na Mungu, na tukapata ushindi mkubwa. Sasa, ni lazima tuanze na Mungu ili safari yetu iendelee kuwa salama na yenye mafanikio," Alisema Kafiti.


 "Safari yangu ya kibunge ni lazima kuanza na Mungu, kwani wakati wa kampeni tulianza na Mungu, tukamaliza na Mungu, na tukapata ushindi mkubwa. Sasa tunapozindua majukumu yetu ya kibunge, hatuna budi kumtanguliza Mungu ili safari yetu iwe salama," alisema Mhe. Kafiti.

Kwa upande mwingine Kafiti ameeleza  vipaumbele vyake atakavyoanza navyo katika utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na  miundombinu ya barabara, maji, afya, elimu, na ajira kwa vijana.


 "Barabara za Ilemela ni tatizo kubwa. Tunahitaji kuongeza juhudi katika kuboresha miundombinu ya barabara, ambapo mtandao wa barabara zenye lami haizidi kilometa 60. Tunaiomba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutusaidia katika hili," Alisema Kafiti.

Aidha, alieleza changamoto ya maji, ambapo alisema kuwa kazi kubwa inayofanyika ni kuboresha chanzo cha maji cha Kibangaja ili kukidhi mahitaji ya wananchi. 

"Ikiwa chanzo hiki kikikamilika, Ilemela itakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 200 za maji, wakati mahitaji yetu ni lita milioni 80. Hii itakuwa ziada ya hali ya juu," Alisema Kafiti.

Hata hivyo, Kafiti alizungumzia umuhimu wa kuboresha sekta ya afya kwa kujenga miundombinu bora na kuajiri wahudumu wa afya wengi ili kuhakikisha wananchi wanapata matibabu bora, akisisitiza pia umuhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa na kusema kuwa serikali itahakikisha elimu inaboreshwa na nafasi za ajira kwa vijana zitatengenezwa.


Baadhi ya viongozi wa dini walieleza kuwa Mhe. Kafiti ameleta kusanyiko la baraka mwanzo wa mwaka kabla hajaanza kutekeleza majukumu yake ya kibunge, na walimpongeza kwa kuchagua kumtanguliza Mungu katika kila hatua ya utumishi wake.

 "Tumemsihi na kumuomba Mungu ampe nguvu za kutenda haki na kuwahudumia wananchi kwa njia inayostahili," walisema viongozi hao.




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3