Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MSANII SHILOLE APATA AJALI AKITOKA KIGOMA

MSANII SHILOLE APATA AJALI AKITOKA KIGOMA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Msanii maarufu na mjasiriamali, Shilole Abdul, amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia leo katika eneo la Malagarasi, mkoani Kigoma, alipokuwa safarini akirejea Dodoma baada ya kuhudhuria sherehe za Mwaka Mpya.

Shilole alikuwa miongoni mwa wageni waliokuwa wamealikwa kwenye sherehe hizo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mheshimiwa Cleyton Chipando (Baba Levo). Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mheshimiwa Chipando kupitia mitandao ya kijamii, gari aina ya Alphard alilokuwa akisafiria Shilole lilipata ajali baada ya kugonga ng’ombe barabarani katika eneo la Malagarasi.

Mbunge Chipando ameandika kuwa Shilole alipata ajali hiyo alipokuwa akiondoka Kigoma kurejea Dodoma, na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Tabora, huku hali yake ikifuatiliwa kwa karibu na madaktari.


Matukio Daima Media,Familia, marafiki, mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wa sanaa wameendelea kumuombea Shilole apone haraka na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Tunamtakia nafuu ya haraka, na tutaendelea kufuatilia maendeleo ya afya yake na kuwajuza pindi taarifa mpya zitakapopatikana.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3