RAIS TRUMP AONYA COLOMBIA
Jan 4, 2026
Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa operesheni ya hivi karibuni dhidi ya Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, iwe funzo kwa dunia nzima akionya kuwa viongozi wengine wa Amerika ya Kusini, akiwemo Rais wa Colombia, Gustavo Petro, wanaweza kukumbwa na hatua kama hiyo kutoka Marekani.
Amedokeza uwezekano wa kuchukua hatua kali dhidi ya utawala wa Petro, akidai kuna dalili za "sera hatarishi kwa usalama wa kikanda na maslahi ya Marekani."
Trump hakufafanua aina ya hatua zitakazochukuliwa, lakini kauli yake imeibua mijadala mikali kuhusu uhusiano wa Marekani na mataifa ya Amerika Kusini, huku wachambuzi wakionya kuwa mivutano hiyo huenda ikaathiri diplomasia ya kikanda.
