Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SIRRO ATOA MAAGIZO UJENZI SOKO LA MWANGA

SIRRO ATOA MAAGIZO UJENZI SOKO LA MWANGA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu  wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa  ujenzi wa soko la Kimkakati la Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kuhakikisha mradi huo unakamilika kufikia mwezi Mei mwaka huu.


Balozi Sirro ametoa maagizo hayo alipofanya ziara kutembelea na kukagua mradi huo na kusema kuwa mradi huo unalipaswa kuwa umekamilika mwezi Desemba mwaka jana hivyo hataakubaali kuona muda aaliotoa unapita na soko halijakaamilika.



Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa serikali inapoahidi na kutoa taarifa kwa wananchi ni lazima jambo hilo litekelezwe na lipo kwenye mkataba hivyo wakandarasi wasiwe sababu ya kuwagombanisha serikali na wananchi wake, kwamba watu wanalisubiri sana hilo soko hivyo lazima muda ulioongezwa utumike kukamilika mradi huo.

Awali Msimamizi wa mradi huo, Joseph Marandu kutoka kampuni ya Asabhi Compay Ltd  inayoshirikiana na Pioneer  Builders Ltd alisema kuwa mradi huo wa miezi 12 ulipaswa kukamilika Desemba 31 mwaka jana lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kukamilisha kwa wakati.


Kufuatia maelezo hayo Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akatoa maagizo ya serikali kuhusu utekelezaji wa mradi huo




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3