Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
UVCCM KIBAHA MJINI  WASEMA WIZARA YA VIJANA MKOMBOZI KWAO

UVCCM KIBAHA MJINI WASEMA WIZARA YA VIJANA MKOMBOZI KWAO

 


Na Matukio Daima Habari blog Kibaha

VIJANA wasema kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana ni mkombozi kwao kwani changamoto zao zitatatuliwa kwa haraka.

Hayo yamesemwa na Katibu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM) kata ya Tangini Wilaya Kibaha Mjini Mkoa wa Pwani Lazaro Benjamin alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.


Benjamin amesema kuwa wanamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara hiyo ambapo ilikuwa ni hitaji la muda mrefu kwa Vijana.


"Vijana sasa watakuwa na mahali ambapo watapeleka changamoto zao na zitapatiwa ufumbuzi kwani ujumbe utafika moja kwa moja hautapita sehemu nyingine,"amesema Benjamin.


Amesema vijana wanahitaji kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao hivyo Wizara hiyo imekuja wakati sahihi na itakuwa ni sehemu ya ukombozi kwa vijana.


"Tunaendelea kupeleka hoja mbalimbali za vijana kupitia mabaraza ya vijana hivyo tunaamini Wizara hii ni jibu la changamoto na kero nyingi za vijana hasa ajira,"amesema Benjamin.


Aidha amewataka viongozi kutenga muda wa kuwa nao karibu ili kuwasikiliza na kuwapa matumaini na kuangalia namna gani ya kutatua changamoto ambazo zinawakabili.


mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3