WAKULIMA WATARAJIA MAKUBWA
Na Mwandishi wetu,
Wakulima wanatarajia makubwa ya hakikisho la uwepo wa Chakula Cha kutosha na Cha akiba kutokana na mazao kustawi kwa wingi shambani na hivyo kutarajia kupata mavuno mengi.
Wakulima wameyasema hayo leo tarehe 16 Januari 2026 mbele ya Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu alipo watembelea Wakulima Mashambani maeneo ya Kijiji cha Lukuledi B Kata ya Lukuledi kujionea hali ya Kilimo na kusikiliza na kutatua changamoto zao.
"Sisi Wakulima hatuna mashaka, mazao yamestawi na tunatarajia kupata mavuno mengi sana mvua zikiendelea kunyesha yatakayo pelekea kuwa na Chakula kingi na Cha akiba pia. Kwa ujumla tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pembejeo kama vile Dawa na Mbegu zinazotupa faraja na hakikisho la Kilimo." Alisema Mkulima Yonas Edwin.
Akizungumza na Wakulima mbalimbali Shilatu aliwapongeza Wakulima hao na kuwapa angalizo la kuhifadhi Chakula.