Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANANCHI WAMUUA MGONJWA WA AKILI  KWA KUITWA MWIZI KIMAKOSA USIKU LUKOBE MORO

WANANCHI WAMUUA MGONJWA WA AKILI KWA KUITWA MWIZI KIMAKOSA USIKU LUKOBE MORO

 

Matukio Daima, Morogoro

Tukio la kusikitisha la mauaji  limeutikisa mtaa wa Lukobe,manispaa ya Morogoro, baada ya wananchi wenye hasira kali kumpiga hadi kumuua kijana mmoja aliyedhaniwa kuwa mwizi, kumbe alikuwa ni mgonjwa wa akili.

Marehemu, Hamza Malingumu Hussein (20), aliyetokea Kilosa na kuwa Lukobe kwa Mjomba wake,Nassib Ngwenje, alitoroka nyumbani majira ya saa tisa usiku na kuanza kuzurura mitaani. 

Mjomba wake mwingine Ngwenje Mohamed, amesema kijana huyo alipohojiwa alijibu hovyo kutokana na hali yake ya kiafya.

“Walipomuona hawakumfahamu, wakamhoji, akajibu hovyo ndipo wakamvamia na kumpiga kikatili,” amesema.

Ngwenje ameongeza kuwa familia ilisimuliwa asubuhi kuhusu kisa cha mtu huyo bila kujua ni ndugu yao, na baada ya kumkosa ndani na kwenda eneo la tukio walimkuta amepigwa akiwa hoi.

Hata hivyo alipotaka kukimbizwa hospitali kwa bajaji alifariki akiwa njiani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amekiri kutokea mauaji hayo na kwamba wamewakamata watuhumiwa watano kuhusika.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3