WANANCHI TUMIENI VYANDARUA KUPAMBANA NA MALARIA SIO KUFUGIA KUKU
Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp
WANANCHI mkoa wa Morogoro wametakiwa kutumia vyandarua kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo,ikiwa ni hatua ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Morogoro ni kati ya mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya wingi wa malaria kwenye mikoa 26 na lengo ni kutika kwenye idadi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima alisema hayo wakati wa kikao Cha uhamasishaji kwa viongozi kuhusu mpango wa ugawaji wa vyandarua ngazi ya kaya.
"Sasa nakubaliana na angalizo lililowekwa, tukianza kutumia vyandarua hivi kwa mambo mengine ambayo sio makusidio yake tutakuwa hatujatendea haki zoezi zima na Nia nzuri ya Serikali, tutakuwa wakali sana kwenye hili, unapewa chandarua harafu unatumia sivyo hatutaelewana "alisema Rc Malima.
Malima alisisitisa umuhimu wa kila mwananchi kutumia chandarua kwa ajili ya kujikinga na mbu, badala ya kutumia vyandarua hivyo kwa shughuli nyingine ambazo sio lengwa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema matumizi yasiyo sahihi ya vyandarua yamekuwa changamoto kwa juhudi za Serikali na wadau katika kutokomeza ugonjwa wa malaria,hivyo viongozi wa umma wanapaswa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya vyandarua.
"Lazima tuwe na elimu kwa umma ifanyike kwa wote,agizo langu ni kwa Watendaji wote wa umma lazima wawe na Elimu ya kupambana na malaria,na izungumzwe kwenye vikao vyote,"alisema.