Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
“BAADA YA KUNYIMWA TUZO YA AMANI YA NOBEL SILAZIMIKI TENA KUFIKIRIA AMANI PEKEE.” — DONALD TRUMP

“BAADA YA KUNYIMWA TUZO YA AMANI YA NOBEL SILAZIMIKI TENA KUFIKIRIA AMANI PEKEE.” — DONALD TRUMP

 

Rais wa Marekani Katika barua hiyo iliyotumwa kwa Waziri Mkuu wa Norway, Trump amesema licha ya amani kuendelea kuwa muhimu, sasa anajihisi huru kufikiria kile anachoona kuwa ni maslahi sahihi kwa Marekani na kwamba haoni tena ulazima wa kufikiria amani pekee, kwa sababu hakutunukiwa Tuzo ya amani ya Nobel. Kauli hiyo imetafsiriwa na wachambuzi kama ishara ya sera ya kigeni yenye msimamo mkali zaidi.


Barua hiyo inajiri baada ya viongozi wa Norway na Finland kupinga vikali uamuzi wa Trump wa kutishia ushuru dhidi ya mataifa ya Ulaya yanayokataa kuiruhusu Marekani kuchukua udhibiti wa Greenland - kisiwa kinachojitawala, chenye utajiri wa madini na chenye umuhimu mkubwa wa kimkakati katika eneo la Aktiki.


Trump amerejelea kauli yake kwamba Denmark haiwezi kuilinda Greenland dhidi ya Urusi au China, na kusisitiza kuwa usalama wa dunia hautapatikana bila Marekani kuwa na "udhibiti kamili" wa kisiwa hicho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3