Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 ELON MUSK ATOA HUDUMA YA BURE YA INTERNET VENEZUELA

ELON MUSK ATOA HUDUMA YA BURE YA INTERNET VENEZUELA

Bilionea namba moja Duniani Elon Musk kupitia kampuni yake ya utoaji wa huduma za 'internet' yenye kasi ya juu kwa kutumia 'satellit', ametangaza kutoa huduma hiyo bure kote nchini Venezuela.

Huduma hiyo itatolewa bure kwa muda wa mwezi mmoja (Januari 3 - Februari 3, 2026) ikiwa ni ishara ya kuwaunga mkono wavenezuela baada ya Rais Nicolás Maduro kutiwa nguvuni na Marekani.

Ikumbukwe kuwa, baada ya Trump kuapishwa kuwa Rais wa Marekani, mapema mwaka 2025, Musk alihudumu kama Mshauri Mkuu wa Rais na mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), lakini baada ya kutokuelewana baina yake na Rais Trump, Musk aliondoka katika utawala wa Trump na kurudi kusimamia makampuni yake.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3