Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
GABON WAIFUTA TIMU YA TAIFA

GABON WAIFUTA TIMU YA TAIFA

 


Serikali ya Gabon imechukua hatua kali ya kuisimamisha rasmi Timu ya Taifa ya Soka ya nchi hiyo kufuatia kutoridhishwa na kiwango duni kilichoonyeshwa kwenye michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco.

 Taarifa iliyotolewa Januari 1, 2026, jijini Libreville, imeeleza kuwa kiwango hicho kilikuwa cha kusikitisha na kisicho na heshima kwa taifa, jambo lililopelekea kuvunjwa kabisa kwa benchi la ufundi na kusimamishwa kwa timu hiyo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.


Katika mabadiliko hayo makubwa, wachezaji wakongwe na nguzo muhimu za kikosi hicho, Pierre-Emerick Aubameyang na Bruno Ecuele Manga, wameondolewa rasmi kwenye timu kwa sasa. Hatua hii inaashiria mwanzo wa mabadiliko ya mfumo ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikitegemea uzoefu wa nyota hao kwa muda mrefu katika medani za kimataifa 


Pamoja na kuisimamisha timu, Serikali imelitaka Shirikisho la Soka la Gabon (FEGAFOOT)  kuwajibika kikamilifu na kuchukua hatua stahiki kurekebisha hali hiyo. Serikali imesisitiza kuwa mwenendo wa timu ulikuwa kinyume na maadili na mfano mwema unaotakiwa kuigwa, hivyo inahitajika mikakati mipya ya kurejesha heshima ya soka la nchi hiyo chini ya uangalizi wa  Fifaworldcup

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3