MWANAMKE AREJESHA SHILINGI MILIONI 561 ALIZOPOKEA KIMAKOSA
Jan 2, 2026
Hakika kuna watu na nusu mwanamke mmoja kutoka nchini Nigeria arejesha kiasi cha Shillingi Million 561 ambacho kiliwekwa kimakosa kwenye akaunti yake ya benki
Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hajiya A hakusita kuwasiliana na benki yake mara tu alipogundua kiasi hicho kikubwa cha fedha kwenye akaunti yake, Alisema "Ninajihisi vizuri kurejesha fedha hizo, Mimi ni mama, na mustakabali wa watoto wangu una thamani kubwa zaidi kwangu kuliko chochote, akaongeza, "Hata pamoja na changamoto zote za kifedha nilizonazo, sitaki kula mali isiyonihusu".
Ungekuwa Wewe Ungeirudisha Pesa Hiyo?
#Matukio Daima Habari
