HISTORIA YA IDD AMINI DADA NA UGANDA
Idi Amin alipinduliwa na majeshi ya Tanzania (TPDF) yakishirikiana na waasi wa Uganda chini ya uongozi wa Milton Obote na Yoweri Museveni 1979.
Baada ya kushindwa, Amin alikimbia Uganda akiwa na familia yake na wasaidizi wachache nchini Libya ambako Muammar Gaddafi wa Libya alimpa hifadhi ya muda.
Hata hivyo, kutokana na shinikizo la kimataifa na hali ya kisiasa, Amin hakukaa muda mrefu Libya.
Alihamia Saudi Arabia ambako ilimkubali kuishi nchini kwao kwa masharti maalum kama kutoruhusiwa kujihusisha na siasa,hakuruhusiwa kutoa matamko ya kisiasa ma aliishi chini ya uangalizi wa serikali akipewa makazi Jeddah na serikali ya Saudi Arabia ikagharamia maisha yake.
Aliishi maisha ya faragha na utulivu alioa wake kadhaa na kuishi na baadhi ya watoto wake pia aliwahi kutoa mahojiano machache sana, akitetea utawala wake na kukana mauaji aliyohusishwa nayo.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000, afya yake ilianza kudhoofika alilazwa hospitalini Jeddah kwa muda mrefu na alifariki tarehe 16 Agosti 2003 akiwa na umri wa takribani miaka 78 alizikwa Saudi Arabia, si Uganda kwani Serikali ya Uganda ilikataa kuurudisha mwili wake watu wengi Uganda bado wanamkumbuka kwa ukatili, mauaji, na hofu na wengine humkumbuka kwa utaifa na msimamo mkali dhidi ya ukoloni.
