KAMALA HARRIS AMPINGA VIKALI RAIS TRUMP KUMKAMATA RAIS WA VENEZUELA NA MKEWE
Jan 4, 2026
Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Kamala Harris amekosoa vikali vitendo vya Rais Donald Trump nchini Venezuela, akivitaja kuwa ni kinyume cha sheria, hatari na kuchochewa na malengo ya kisiasa badala ya maslahi ya taifa.
Katika chapisho lenye maneno makali kwenye X, Harris alionya kwamba hatua hiyo inahatarisha kudhoofisha ukanda huo huku ikiweka maisha na rasilimali za Wamarekani hatarini.
Harris alisema umma wa Marekani hauungi mkono vitendo hivyo vya kijeshi na kumshutumu Trump kwa kuwapotosha watu.
Hili si kuhusu madawa ya kulevya au demokrasia. Ni kuhusu mafuta na nia ya Donald Trump kucheza kama gwiji mkuu wa eneo hilo amesema Harris.
Katika mkutano na wanahabari, Trump alisema makampuni makubwa ya mafuta ya Marekani yatatumwa Venezuela ili kujenga upya sekta hiyo.
