URUSI YAITAKA MAREKANI KUMWACHIA HURU RAIS WA VENEZUELA
Jan 4, 2026
Urusi inayoongozwa na Rais Vladimir Putin imeitaka Marekani kumwachilia mara moja Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela, ikiyataja kuwa ni kitendo cha 'uchokozi wa silaha' na ukiukwaji wa sheria za kimataifa.
Maafisa wa Urusi walisema kuwa Washington haina mamlaka ya kisheria ya kumshikilia kiongozi aliyepo madarakani na wakaonya kuwa hatua hiyo inaweza kuvuruga utulivu wa ukanda huo.
Tamko hilo linakuja wakati athari za kimataifa zikizidi kuongezeka baada ya hatua za Marekani nchini Venezuela, huku Moscow ikiishutumu Marekani kwa kudhoofisha uhuru wa mataifa na kuweka mfano hatari.
