Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KAMPUNI YA MAFUTA YA MAREKANI KUANZA KUFANYA KAZI VENEZUELA-TRUMP

KAMPUNI YA MAFUTA YA MAREKANI KUANZA KUFANYA KAZI VENEZUELA-TRUMP

 


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa sekta ya mafuta ya Marekani inaweza kuanza kufanya kazi kikamilifu nchini Venezuela ndani ya kipindi cha miezi 18, kufuatia operesheni ya kushtukiza ya kijeshi iliyoondoa madarakani Rais Nicolás Maduro.

Akizungumza na NBC News, Trump alisema kiasi kikubwa cha fedha kitatumika kufufua sekta hiyo, huku makampuni ya mafuta yakitarajiwa kugharamia awali kabla ya kurejeshewa fedha na serikali ya Marekani au kupitia mapato yatakayopatikana.

Aidha, wawakilishi wa makampuni makubwa ya mafuta ya Marekani wanatarajiwa kukutana na utawala wa Trump wiki hii, kwa mujibu wa taarifa ya CBS News.

Hata hivyo, wachambuzi walioliambia shirika la BBC wamesema kurejesha uzalishaji wa zamani wa mafuta wa Venezuela kunaweza kugharimu makumi ya mabilioni ya dola na kuchukua hadi muongo mmoja.

Trump amesisitiza kuwa kuwa na Venezuela kama mzalishaji mkubwa wa mafuta kutasaidia kushusha bei ya mafuta duniani, jambo litakaloinufaisha Marekani. Wachambuzi bado wana shaka kama mpango huo utaathiri kwa haraka soko la kimataifa, wakisema wawekezaji watahitaji uthabiti wa kisiasa kabla ya kuwekeza kwa kiwango kikubwa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3