Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAFURIKO TINDIGA YAWAACHIA MACHUNGU WANANCHI, KILOMBERO SUGAR YAWAFIKIA

MAFURIKO TINDIGA YAWAACHIA MACHUNGU WANANCHI, KILOMBERO SUGAR YAWAFIKIA

 

Matukio Daima. Kilosa

WANANCHI wa kata ya Tindiga wilayani Kilosa mkoani Morogoro waliofikwa na athari za mafuriko makubwa yaliyosababisha uharibifu wa mali na kuathiri mamia ya familia, wameendelea kufikiwa na misaada ya mahitaji ya kibinadamu kutoka kwa wadau wa maendeleo ikiwemo kampuni ya sukari ya Kilombero sugar.

Msaada huo wa kibinadamu ni hatua ya kuonesha mshikamano, ambapo Kilombero Sugar wametoa msaada wa sukari tani tano wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza makali ya maisha kwa waathirika wa mafuriko hayo.

Msaada huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Bw.Shaka Hamdu Shaka na kukabidhiwa rasmi na Victor Baberwa kwa niaba ya uongozi wa Kampuni ya Kilombero Sugar.

DC Shaka amepongeza hatua hiyo na kusisitiza kuwa bado mahitaji ni makubwa na kutoa wito kwa wadau wengine, mashirika ya kijamii, makampuni na watu binafsi kujitokeza kuwasaidia waathirika hao kwa chakula, mavazi na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu.

Taarifa zinaeleza kuwa jumla ya kaya 202 zimeathirika na zaidi ya wananchi 1,411 wamekumbwa moja kwa moja na janga hilo.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3