MAPOROMOKO YA MTO ENDORO NI MOJA YA VIVUTIO VILIVYOMO NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO
Na,Jusline Marco;Arusha
Maporomoko ya maji Endoro yaliyopambwa na msitu uliosheheni sauti za ndege na kupambwa na ulinzi wa Wanyamapori mbalimbali, haya ni maporomoko ya aina yake na hapa hupaswi kuwa na mtazamo wa wahenga kwamba Chema chajiuza na kibaya chajitembeza.
Maporomoko haya ya maji Endoro ni eneo zuri lililopo kusini ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, takribani kilomita 6.5 kutoka mji wa Karatu, njia ya kuelekea maporomoko haya hupitia msitu na Mapango ya Tembo na huchukua takribani saa 2 Hadi 3 za matembezi ya wastani.
Mto Endoro hutiririsha maji mwaka mzima kutoka kwenye kingo za korongo, ukilishwa na chemchem za asili kutoka nyanda za juu za Ngorongoro na kuanguka kwa urefu wa zaidi ya mita 40, njia ya kuelekea kwenye maporomoko hayo hupitia sehemu ya msitu wa nyanda za juu kaskazi katika hifadhi ya Ngorongoro ambapo wapenda ndege na wanyamapori wakubwa kama tembo, nyati na nguruwe pori, Simba na wanyama wengine watakapopanda watakuwa na kumbukumbu isiyosahaulika.
Hayo ni maporomoko ya maji ya Endoro ukifika huko utatamani uoge maji hayo.



