Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RC BABU AGEUKA MBOGO KUCHELEWA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MADARASA..

RC BABU AGEUKA MBOGO KUCHELEWA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MADARASA..

 

MWANGA.

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amemwagiza Katibu Tawala mkoa huo, Kiseo Nzowa kuwachukulia hatua wale wote waliochelewesha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Muungano wilayani Mwanga. 

Babu alitoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya elimu katika wilaya ya Mwanga ambapo alishangazwa kuona shule hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo mawili Aprili 19 mwaka jana lakini mpaka sasa ujenzi upo hatua ya msingi. 

"Haiwezekani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anapambana kuleta fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu pamoja na kuhakikisha watoto wanasomea katika mazingira mazuri alafu watokee watu wachache wamkwamishi hili hatuliungi mkono nakuagiza Katibu Tawala yoyote aliyeshiriki katika uzembe huu achukuliwe hatua" Alisema Babu.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3