Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA WAPATA TABASAMU BAADA YA AL SAEDY KUTOA MSAADA

WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA WAPATA TABASAMU BAADA YA AL SAEDY KUTOA MSAADA

 

Na Matukio Daima, Kilosa.

Hatimaye tabasamu limeanza kurejea kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa waliokumbwa na mafuriko, baada ya kampuni ya mabasi ya Al Saedy kujitokeza na kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa waathirika wa janga hilo.


Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, unahusisha magodoro zaidi ya 100, mifuko 100 ya unga wa sembe, sabuni za kufulia pamoja na maji ya kunywa, ambavyo vitasaidia kupunguza makali ya maisha kwa wananchi waliopoteza mali zao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema msaada huo ni faraja kubwa kwa waathirika wengi ambao wameathirika kwa kiwango kikubwa baada ya mashamba na makazi yao kuharibiwa na mafuriko.

Mafuriko hayo yalitokana na mvua kubwa zilizoendelea kunyesha katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Manyara, na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kilosa.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3