SERIKALI YA UGANDA YAKANUSHA MADAI YA BOBE WINE KUWEKWA KIZUIZINI
Jan 16, 2026
SERIKALI ya Uganda imekanusha madai kuwa Kiongozi wa upinzani Bobi Wine amewekwa katika kizuizi cha nyumbani kufuatia Uchaguzi Mkuu.
Msemaji wa Polisi Kituuma Rusoke alisema Wine analindwa kwa sababu si raia wa kawaida," akiongeza kuwa uwepo wa Polisi nje ya nyumba yake na vikwazo vya harakati zake ni kwa sababu za usalama.
Mzozo huo unakuja huku matokeo ya Uchaguzi wa mapema yakionyesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa tofauti kubwa huku akitaka kurefusha utawala wake wa takribani miongo minne.
Kura hiyo ilifuatia kampeni ya mvutano iliyoambatana na kuzimwa kwa intaneti, matatizo ya kiufundi katika vituo vya kupigia kura, na madai ya ukandamizaji.
