SIRRO ATOA MAAGIZO UJENZI SOKO LA MWANGA
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa soko la Kimkakati la Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kuhakikisha mradi huo unakamilika kufikia mwezi Mei mwaka huu.
Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa serikali inapoahidi na kutoa taarifa kwa wananchi ni lazima jambo hilo litekelezwe na lipo kwenye mkataba hivyo wakandarasi wasiwe sababu ya kuwagombanisha serikali na wananchi wake, kwamba watu wanalisubiri sana hilo soko hivyo lazima muda ulioongezwa utumike kukamilika mradi huo.
Awali Msimamizi wa mradi huo, Joseph Marandu kutoka kampuni ya Asabhi Compay Ltd inayoshirikiana na Pioneer Builders Ltd alisema kuwa mradi huo wa miezi 12 ulipaswa kukamilika Desemba 31 mwaka jana lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kukamilisha kwa wakati.
Kufuatia maelezo hayo Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akatoa maagizo ya serikali kuhusu utekelezaji wa mradi huo




