Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
UJUE UTAJIRI WA VENEZUELA

UJUE UTAJIRI WA VENEZUELA

 


Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro anashikiliwa na vikosi vya Marekani kufuatia oparesheni kubwa ya kijeshi iliyofanywa na Marekani nchini humo.


Zifuatazo ni dondoo muhimu kuhusu utajiri wa Venezuela ambao kwa muda mrefu umekuwa hauwanufaishi wananchi wake wanaoendelea kuwa maskini.


- Venezuela ina hifadhi ya takribani mapipa bilioni 303 ya nishati ya mafuta na ndiyo hifadhi kubwa zaidi duniani.


- Ukiilinganisha Venezuela na nchi nuingine duniani zinazozalisha mafuta, Venezuela ina mapipa bilioni 303, Saudi Arabia ina mapipa bilioni 267, UAE ina mapipa bilioni 113, Kuwait ina mapipa bilioni 102 na Nigeria ina mapipa bilioni 37.


-Venezuela ina utajiri wa gesi asilia takribani mita za ujazo trilioni 6, ina dhahabu takribani tani 8,000, chuma takribani tani bilioni 2, makaa ya mawe, almasi na madini ya Bauxite.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3