MUSEVENI AONGOZA MATOKEO YA AWALI YA URAIS KWA ASILIMIA 7
Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza matokeo ya awali yanayoonyesha Rais Yoweri Museveni akiendelea kuongoza ASILIMIA 76.25
katika kinyang'anyiro cha urais kwa kupata asilimia 76.25 ya kura, sawa na takribani kura milioni 3.9. Matokeo hayo yametolewa hadi kufikia asubuhi ya leo, baada ya asilimia 45 ya vituo vya kupigia kura kuwasilisha taarifa zao.
Kwa mujibu wa Tume hiyo, mpinzani wake mkuu kutoka upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amejipatia asilimia 19.85 ya kura, ambazo ni takribani kura milioni 1.3, na hivyo kushika nafasi ya pili.
Tume ya Uchaguzi imesema mchakato wa kuhesabu na kuhakiki kura bado unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku ikieleza kuwa matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa kesho baada ya taratibu zote kukamilika
