Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MTUMISHI WIZARA YA MAJI, MKEWE NA MTOTO WATEKETEA KWA MOTO

MTUMISHI WIZARA YA MAJI, MKEWE NA MTOTO WATEKETEA KWA MOTO

 


WATU  watatu wa familia moja wamefariki dunia katika eneo la Nyarusurya, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba yao waliyokuwa wamelala usiku wa kumakia leo.

Akizungumza kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara, Augustin Magere amesema moto huo ulianzia sebuleni na kusambaa kwa kasi hadi kwenye vyumba vinne vya nyumba hiyo, hali iliyosababisha vifo vya watu watatu Baba mama na mtoto.

Magere amemtaja aliyefariki Baba mwenye nyumba Rochi Shaban (39) alikuwa Meneja wa ubora wa Maji Mkoa wa Mara na mke wake Mariam George Msigwa (34) na Mtoto Rouch Mkole (4) chanzo cha Moto hakijajulikana hadi sasa.

Wakizungumza baadhi ya majiran walisema moto huo ulianza kuwaka majira ya Usiku ndio walipoamka nakwenda kuuzima huku wakiomba msaada wa Zimamoto lakini hawakufanikiwa kutokana na ukubwa wa Moto huo.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3